Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya uteuzi wa
wajumbe kuunda kamati mbili za awali za haki, na kamati mbili za rufani za
vyombo hivyo.
Rais
wa zamani wa Yanga, Tarimba Abbas ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ataongoza
Kamati ya Nidhamu. Wajumbe wanaounda kamati hiyo ni Wakili Jerome Msemwa (Makamu
Mwenyekiti), Kassim Dau, Nassoro Duduma na Kitwana Manara.
Kamati
ya Rufani ya Nidhamu inaendelea kuongozwa na Profesa Mgongo Fimbo wakati makamu
wake ni Wakili Hamidu Mbwezeleni. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Titus
Bandawe, Twaha Mtengera na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface
Mpaze.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria anaongoza Kamati
ya Maadili. Wajumbe ni Wakili Ezekiel Maganja, Wakili Victoria Mandari, Kanali
mstaafu Enos Mfuru na Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Said Mtanda.
Kamati
ya Rufani ya Maadili inaundwa na Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti),
Wakili Alesia Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na
Chabanga Hassan Dyamwale.
TFF, CRDB
KUTATHIMINI TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeagiza kifanyike
kikao cha dharura kati ya Sekretarieti ya TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
na benki ya CRDB ili kutathimini maendeleo ya matumizi ya tiketi za
elektroniki.
Lengo
la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa mfumo huo wa tiketi
za elektroniki ni kutafuta ufumbuzi pamoja changamoto zake.
Viwanja
vinane nchini vimefungwa mfumo huo wa tiketi za elektroniki. Viwanja hivyo ni Uwanja
wa Azam uliopo Chamazi, Uwanja wa Kaitaba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Uwanja
wa Jamhuri, Morogoro, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Uwanja wa Sheikh Kaluta
Amri Abeid, Uwanja wa Mkwakwani, na CCM Kirumba.
MECHI YA
STAND, KANEMBWA MEZANI TENA
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo
hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada
ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka
jana mjini Shinyanga.
Mechi
hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya
kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia
Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la
Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi
wa mechi hiyo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment