Timu
ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi ya marudiano
ya raundi ya kwanza ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia (Shepolopolo)
itakayochezwa Ijumaa (Februari 28 mwaka huu).
Twiga
Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage na Msaidizi wake Nasra Juma inaendelea
vizuri, na kwa mujibu wa programu ya benchi lao la ufundi kesho (Jumatatu),
Jumanne na Jumatano itafanya mazoezi saa 10 jioni.
Mazoezi
hayo yatafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam. Uwanja huo ndiyo utakaotumika kwa ajili ya mechi hiyo
itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Shepolopolo
ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-1 wiki iliyopita inatarajiwa kuwasili nchini
Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet, na siku hiyo hiyo
itafanya mazoezi Azam Complex.
Waamuzi
wa mechi hiyo Ines Niyonsaba, Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis
Iratunga, wote kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano.
YANGA, PRISONS
KUPANGIWA TAREHE MPYA
Mechi
namba 118 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Tanzania Prisons
iliyokuwa ichezwe Februari 26 mwaka huu itapangiwa tarehe nyingine.
Uamuzi
wa kuiondoa mechi hiyo iliyokuwa ichezwe Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam umefanywa ili kuipa fursa zaidi Yanga kujiandaa kwa mechi yake ya
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Ahly ya Misri itakayofanyika Jumamosi (Machi 1
mwaka huu).
Al
Ahly na Yanga zitarudiana wiki moja baadaye kati ya Machi 7, 8 au 9 mwaka huu
jijini Cairo, Misri.
MECHI ZA
MABORESHO TAIFA STARS
Mechi
za mpango wa kuboresha Taifa Stars kati ya mikoa na mikoa wiki hii itakuwa kama
ifuatavyo;
Februari
25 Njombe vs Ruvuma (Uwanja wa Njombe)
Kinondoni vs Ilala (Uwanja wa
Karume)
Februari
26 Morogoro vs Pwani (Uwanja wa Jamhuri)
Geita vs Kagera (Uwanja wa
Geita)
Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja
wa Ushirika)
Iringa vs Mbeya (Uwanja wa
Samora)
Shinyanga vs Simiyu (Uwanja wa
Kambarage)
Lindi vs Mtwara (Uwanja wa
Ilulu)
Februari
27 Temeke vs Kinondoni (Uwanja wa Karume)
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment