KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Friday, April 18, 2014

MAMA SALMA APOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO-ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI.

  Bwana Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo  ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.
 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja  kilichoko katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano .
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo.
 Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele (PICHA NA JOHN LUKUWI).

No comments: