-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku
Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu
ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Fatma Karume akipokea Nishani ya
Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman
Karume Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano
Daraja Nne wakati wa hafla ya kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano
zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mama Maria Nyerere akipokea nishani ya
kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana usiku ametunuku
nishani na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao
86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa Tanganyika na
Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku
Rais mstaafu wa Awamu ya tatu Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu
ya miaka 50 ya Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha
na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment