KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, May 14, 2014

KINANA ALIVYOPIGA KAZI WILAYA YA UYUI MKOANI TABORA, MAMIA WAHUDHURIA MIKUTANO YAKE YA HADHARA.

 Mamia ya wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa habdhara leo Mei 12, 2014, katika kijiji cha Kizengi, Wilayani Uyui akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya uzitatua katika mkoa wa Tabora.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mamia ya wananchikatika mkutano wa hadhara leo Mei 12, 2014, katika kijiji cha Kizengi, Wilayani Uyui Nape hupo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Kinana ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya uzitatua katika mkoa wa Tabora.
Mwananchi mwenye hamasa akishangilia wakati wa mkutano huo wa hadhara uliohutubia na Katibu Mkuu wa CCM Kinana katika kijiji cha Kizengi.
 Katibu Mkuu wa CCM akisindikizwa kwa ngoma nderemo na hoihoi wakati akienda kwenye Ofisi ya CCM Kata ya Kizengi, hutubia mkutano wa hadhara, Mei 12, 2014.
Vijana wakiselebuka kwa ngoma ya asili ya Unyemwezini kumlaki Kinana alipowasili Kizengi, wilayani Uyui mkoani Tabora,Mei 12, 2014.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akitazama vitabu alipotembelea maktaba ya shule ya Sekondari ya Loya, Uyui mkoani Tabora  Mei 12, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mkutano wa hadhara kijiji chga  Loya wilayani Uyuwi mkoani Tabora, Mei 12, 2014
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara kijiji chga  Loya wilayani Uyuwi mkoani Tabora,Mei 12, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akisalimia wachezaji wa timu ya kata ya Loya, Uyui mkoani Tabora alipowasili kwenye Kata hiyo,Mei 12, 2014. Kulia ni Mbunge wa Igalula Athuman Mfutakamba na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Mussa Ntimiza
Kamisaa wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye mkutano wa hadhara wa Loya
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akitoka katika jengo la Ofisi ya CCM kaya ya Loya, wilaya ya Uyui mkoani Tabora, baada ya kuzindua ujenzi wa Ofisi hiyo, Mei 12, 2014.
"Nataka kuwa Mbunge nisaidie wananchi"  Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape, akimsikiliza mwnafunzi Ngassa Shigela wa kidato cha III katika shule ya Sekondari  Lutende, Uyuwi, Tabora, alipokutana na mwanafunzi huyo wakati Katibu Mkuu wa CCM Kinana alipokangua nyumba tatu za walimu wa shule hiyo. Nape yupo katika msafara wa Katibu Mkuu huyo.
Katibu Mkuu, Kinana akizungumza baada ya kukagua nyumba za walimu shule ya sekondari ya Lutende, Uyuwi
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi na wanaCCM wa Uyuwi kwenye shule ya sekondari Lutende.Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments: