Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Sarah
Brown, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza na Mwenyekiti Mtendaji wa Global
Business Coalition for Education muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa
‘Getting Serious About Results: The Grand Convergence of Education and Health”
ulioandaliwa na Taasisi ya Mama Sarah Brown kwa kushirikiana na Umoja wa
Mataifa. Mkutano huo umefanyika huko New York.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Sarah
Brown, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza na Mwenyekiti Mtendaji wa Global
Business Coalition for Education muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa
‘Getting Serious About Results: The Grand Convergence of Education and Health”
ulioandaliwa na Taasisi ya Mama Sarah Brown kwa kushirikiana na Umoja wa
Mataifa. Mkutano huo umefanyika huko New York.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana
na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Bwana Gordon Brown kabla ya kuanza mkutano
uliozungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana duniani.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dk. Sarah
Maongezi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Taasisi ya WAMA muda mfupi kabla
kuanza mkutano huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano
wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and
Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani.
Mkutano huo ilifanyika huko New York
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano
wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and
Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani.
Mkutano huo ilifanyika huko New York
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano
wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and
Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani.
Mkutano huo ilifanyika huko New York.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa mkutano uliojadili masuala ya elimu na
afya kwa vijana duniani huku viongozi wengine mashuhuri wakisubiri kuzungumza.
Kushoto kwa Mama Salma ni Dkt. Rajiv Shah, Afisa Mtendaji kutoka USAID,
akifuatiwa na Bwana Mark Dybul, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Fund to fight
AIDS na wa mwisho ni Bwana V. Shanker, Afisa Mtendaji Mkuu wa Afrika, Mashariki
ya Kati, Ulaya na Marekani kutoka Standard Chartered.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Dkt. Andy Shih, Makamu wa Rais Mwandamizi anayeshughulikia
masuala ya sayansi kutoka katika Shirika la ‘Autism Speaks” (masuala ya usonji)
wakati mgeni huyo alipomtembelea Mama Salma kwenye hotelin aliyofikia huko New
York, nchini Marekani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo
na Dkt. Andy Shih.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi Dkt. Andy Shih jarida la
WAMA mara baada ya kufanya mazungumzo ya ushirikiano baina ya Taasisi zao.(PICHA NA JOHN LUKUWI).
Nchi zinazoende lea zinakabili wa na changamoto ya upatikanaj i wa fursa za elimu kwa watoto wenye umri wa kwenda shule
Na Anna Nkinda –
Maelezo, New York
Nchi za
Mashariki na Kusini mwa Afrika ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya
upatikanaji wa fursa za elimu kwa watoto wenye umri wa kwenda shule, ubora na
usahihi wa elimu, masuala mtambuka kama Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ugonjwa wa
Ukimwi.
Changamoto nyingine ni
upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana na udahili
mchache wa wasichana katika masomo ya sayansi.
Hayo yamesemwa leo na
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea katika majadiliano ya elimu na
afya kwa vijana yaliyoandaliwa na Umoja wa kimataifa wa Taasisi za Biashara kwa
ajili ya Elimu na kufanyika katika Hoteli ya Reed Smith mjini New York.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwa upande wa
sekta ya afya ina changamoto ambazo zina uhusiano mkubwa na elimu na kutoa
mfano wa vifo vya akina mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi, vifo vya
watoto, ndoa za utotoni, mimba katika umri mdogo, utapiamlo na upungufu wa
nguvu kazi.
Alisema Serikali na
wananchi wa Tanzania walitambua mapema umuhimu wa kuwekeza kikamilifu katika
elimu kama msingi wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia hususan lengo la pili
linalohusu Elimu kwa wote.
“Serikali yetu
ilianzisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu
ya Msingi na mpango wa maendeleo ya
Elimu ya Sekondari. Mipango yote hii miwili ina malengo ya kuongeza upatikanaji
wa elimu bora kwa watoto wote walio katika umri wa kwenda shule, kuongeza ubora
na usahihi wa elimu.
Kuboresha urari wa
kijinsi na walimu na ufundishaji, kuongeza tija katika uongozi na utawala bora,
kurasimisha masuala mtambuka kama vile UKIMWI, Elimu ya Stadi za Maisha, elimu ya mazingira na jinsia”, alisema Mama
Kikwete.
Alisema
mpango wa matokeo makubwa sasa katika
elimu unalenga kujenga uwezo wa walimu kwa kutoa mafunzo ya pahala pa kazi, kusaidia
watoto wasiofanya vizuri kwa kuandaa vitendea kazi mahususi vinavyozingatia
umri na mahitaji, kuboresha miundo mbinu, kwa kujenga madarasa, maabara na
nyumba za walimu.
Kuboresha vifaa vya ufundishaji kama vile madawati, vifaa vya
maabara, kemikali na kutoa vitu vya
kuongeza motisha kwa walimu.
Mwenyekiti huyo wa WAMA
alimalizia kwa kusema elimu bora itapatikana ikiwa afya za vijana zitaboreshwa na
kuwa na mikakati ambayo inatambua uhusiano mkubwa wa masuala hayo kwani bila ya
elimu timilifu ni vigumu kufikia malengo yaliyopo.
Kwa upande wake Mke wa
waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mama Sara Brown ambaye ni Mwenyekiti
Mtendaji wa Umoja wa kimataifa wa Taasisi za Biashara alimpongeza Mama Kikwete
kwa kazi anayoifanya ya kutoa elimu kwa watoto wa kike ambao ni yatima na
wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuboresha afya ya mama na mtoto.
“Nilitembelea nchini
Tanzania mwaka 2007 na kujionea kazi anayoifanya Mama Kikwete nampongeza kwa
hili. Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu na afya bora ili
waweze kuwa na maisha bora hapo baadaye”, alisema Mama Brown.
Nao wachangia mada
katika mjadala huo walisema ni muhimu watoto wa kike wakapata elimu sawa na
watoto wa kiume kwani wakipata elimu unyanyasaji wa kijinsia ambao unazidi
kuongezeka dhidi yao utapungua na kutakuwa na usawa katika mambo mengi.
Walisema, “Wafadhili
mbalimbali wamekuwa wakiwekeza katika afya na elimu hasa kwa watoto wa kike ili
kuwajengea mazingira mazuri ya kusoma ikiwa ni pamoja na kuwajengea madarasa na
vyoo. Ni vyema vijana wakapata elimu na afya bora ili waweze kujihusisha na
shughuli za maendeleo”.
Mkutano huo ni
moja ya maandalizi ya Mkutano wa 69 wa baraza
kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaotarajiwa kufunguliwa tarehe 24/9/2014 mjini humo.
No comments:
Post a Comment