Washiriki
kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi
wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Speke Munyoyo Kampala, Uganda. Kushoto
ni Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda,
katikati ni Meneja wa Takwimu za Kilimo Titus Mwisomba kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile.
Washiriki wengine
kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi
wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Speke Munyoyo Kampala, Uganda. Kushoto
ni Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya akifuatiwa na Dk. Camilius
Kasalla kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akimpongeza
Mwandishi wa Kitabu cha Mapinduzi ya Takwimu Afrika Prof. Ben Kiregyera baada
ya kukizindua kwenye Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika
uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.
Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akiwahutubia
washiriki mbalimbali kutoka barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa
Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Speke Munyoyo Kampala, Uganda. (PICHA NA
VERONICA KAZIMOTO - KAMPALA)
No comments:
Post a Comment