KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Monday, January 19, 2015

WAJUMBE WA ARSENAL WATUA NCHINI

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula (kushoto), Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey (kulia) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Arsenal, Sam Stone
  Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey akifafanua jambo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Arsenal, Sam Stone.  
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Arsenal, Sam Stone.  
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa Arsenal, Sam Stone akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu fursa za kufanya biashara za kuuza vifaa vya michezo vya klabu hiyo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na makampuni ya Tanzania. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula na Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey.   

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup, Imani Kajula akizungumza na waandishi wa habari.
Mwandishi wa Habari za Michezo, Zahoro Milanzi akipokea zawadi ya jezi harisi ya klabu ya Arsenal kutoka kwa Meneja Maendeleo wa Arsenal, Daniel Willey. 

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Arsenal imepanga kutuma maofisa biashara wake jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano na wafanyabiashara kadhaa wakubwa nchini Tanzania.

Huu utakuwa ujumbe wa kwanza kabisa wa Arsenal nchini Tanzania, ambapo klabu hii kubwa ya Uingereza inataka kujenga ushirika mkubwa kabisa katika maeneo ya masoko na chapa zake, ili kutanua mafanikio yaliyofikiwa kwenye nchi nyingine za Afrika kama Kenya, Uganda na Nigeria.

Washika Bunduki hao wa London wanataka kutoa fursa kwa benki za Tanzania pamoja na kampuni za simu na taasisi nyingine kuweza kupata rasilimali zihusianazo na Arsenal, kama vile bidhaa zilizosainiwa kwa majina ya wachezaji, tiketi za mechi.

Arsenal wanasema kwamba wanaweza kuwapatia washirika wao hao uwanja mpana wa masoko kwa ajili ya kuwasaidia kutimiza malengo mbalimbali ya kibiashara.

Ofisa Biashara Mkuu wa Arsenal, Vinai Venkatesham amesema kwamba wameichagua Tanzania kwa sababu wana washabiki wengi, na kwa kushirikiana na taasisi za Tanzania, watakuwa karibu zaidi na washabiki wao kuliko ilivyokuwa awali.

"Katika bara lenye nchi zaidi ya 50, tumechagua kuzuru Tanzania kimkakati kwa sababu tunaiamini nchi hiyo. Arsenal ina mamilioni ya Watanzania ambao ni washabiki waaminifu na wenye mapenzi makubwa nayo.

"Kwa kushirikiana na taasisi za huko, tutaweza kuisogeza klabu karibu zaidi na washabiki hao kuliko ilivyokuwa awali, huku tukizipatia taasisi husika fursa pekee za kuifikia klabu yetu," akasema Venkatesham.

Wajumbe hao wa jopo la Maendeleo ya Ushirikiano ya Arsenal wanatarajia kuwasili nchini Tanzania Januari 18 mwaka huu, ambapo watakaa kwa wiki moja jijini Dar es Salaam, kuitisha mikutano kadhaa ya awali ya kibiaashara na kuzindua rasmi mchakato wa kutafuta washirika wa kwanza kabisa nchini Tanzania.

No comments: