Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 26/01/2015
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilisaini mkataba maalum na timu ya
Real Madrid ya Nchini Hispania ya
kuanzisha na kuendesha kituo cha michezo (NSSF-
REAL MADRID Sports Academy) kwa lengo la kuibua, kuendeleza na kukuza
vipaji kwa mpira wa miguu. Shirika la NSSF litajenga kituo hicho katika eneo la
Mwasonga Kigamboni nje kidogo ya mji wa Dar es Salaam na wataalamu kutoka timu
ya Real Madrid watatoa mafunzo kwa vijana wa umri wa miaka13 hadi 19 kwa
madhumuni ya kukuza mpira wa miguu nchini, kupata wachezaji bora wanaouzika nje
na ndani ya nchi pamoja na kulipatia mapato shirika na nchi kwa ujumla .
Akizungumza na Waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya Habari Nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dr. Ramadhani K.
Dau alisema mradi huo ukiwa kama sehemu ya uwekezaji wa NSSF ulianza maramoja
baada ya kusaini mkataba. NSSF imeanza
utaratibu wa kuwabaini vijana walengwa ambapo kwa kuanzia utafutaji wa vipaji
vya mpira wa miguu utaanzia mkoa wa Dar es Salaam kwa vijana wenye umri wa
chini ya miaka 14. Utafutaji wa vipaji utafanyika kiwilaya kwa Wilaya za mkoa
wa dar es salaam na utakuwa unafanyika katika
viwanja vya Karume. Zoezi hilo litakuwa linafanyika kati ya saa 1 asubuhi hadi
saa 9 alasiri kwa tarehe zilizoainishwa.
Uandikishaji wa washiriki utakuwa unafanyika siku za
mwisho wa wiki ili kutoathiri wanafunzi watakaopenda kushiriki na utaanza rasmi
tarehe 14 na 15,na tarehe 22 na 23 Februari
2015, na kufuatiwa na michezo ya majaribio tarehe 28 Februari,na Tarehe 1 Machi
2015 kwa wilaya zote za mkoa wa Dar es
salaam ambapo kituo kitakuwa viwanja vya Karume kuanzia saa moja asubuhi hadi
saa 9 alasiri.
Zoezi la Uandikishaji halitahusisha gharama
zozote kwa washiriki, na uandikishaji wa washiriki utafanyika kwa kujaza fomu
maalum na kupewa namba ya ushiriki na kila mshiriki atapata fursa ya kucheza katika
awamu mbili za dakika 30. Kwa kuanzia washiriki watatakiwa kuja na vifaa vyao
vya michezo.
Zoezi la awali litafanywa na wataalam
wa ndani ya nchi ambapo Vijana 500 kati ya wote watakaofanyiwa majaribio wataingia katika awamu ya pili ya majaribio na
watadahiliwa na wataalamu kutoka Klabu
ya Real Madrid na hatimaye kupatikana vijana 30 amabo ndio wataingia
katika shule maalum ya mafunzo kwa awamu
ya kwanza. Wakati wa uandikishwaji washiriki watatakiwa kuja na wazazi/walezi wao
wakiwa na vitambulisho vyao,na kijana husika awe na Cheti halisi cha kuzaliwa na kopi yake pamoja na picha mbili za pasport rangi ya blue.Muda wa uandikishaji na
majaribio unaweza kuongezwa kulinagana na mahitaji.
Shirika la NSSF linatoa wito kwa
vijana kujitokeza kwani ni fursa kwao ya kuweza kujiendeleza kimichezo na
kujiajiri katika tasnia hiyo
No comments:
Post a Comment