NA MWANDISHI WETU
MJI wa Songea jana ulizizima kwa mapokezi makubwa ya viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakiongozwa na
kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe.
Zitto, ambaye ameambatana na viongozi wengine wa juu wa ACT
akiwemo Mwenyekiti wa ACT Taifa, Anna Mghwira pamoja na Katibu Mkuu wake Samson
Mwigamba.
Viongosi hao walisili jana mjini hapa ambapo walilakiwa na mamia ya wananchi wa mji
wa Songea wakiongozwa na vijana wa bodaboda zaidi ya 300.
Akihutubia mamia ya wananchi jana mjini Songea katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi ya Malori Majengo,
Zitto, alisema lengo la kuanza ziara mkoani Ruvuma ikiwa kuenzi na kutekelza
kwa vitendo azimo la Songea.
Alisema na hilo pia mkoa huo una historia ya ukombozi wa
vita ya majimaji iliyoanzia wilayani Kilwa na baadaye kuenea hadi Songea.
Mbunge huyo wa zamani ya Kigoma Kaskazini, alisema kutokana
na hali hiyo ACT-Wazalendo wameanza ziara hiyo ili kupata baraka za mababu wa
ukombozi na si kushindana au kuviponda vyama vingine vya siasa.
Alisema kitendo cha baadhi ya watu kufikiri kuwa ziara yake
ina lengo la mashambulizi si sahihi bali sasa ni changamoto kwa wakazi wa mkoa
wa Ruvuma kuhakikisha wanapanda viongozi wa upinzani kama njia ya kustawisha
demokrasia nchini.
“Ruvuma ni Mkoa ambao hauna mbunge wa upinzani hata mmoja
na tumeona tutume salamu kwa umma huku lengo letu likiwa likiwa kuing’oa CCM
madarakani na kwamba hatuna nia ya kugambana na vyama vingine.
“Wakazi wa Songea ni wajibu wenu kupima je pamoja na historia
ya ukombozi ambayo ACT-Wazalenzo tunaamini ndio misingi ya ukombozi wan chi
yetu je kukosa mbunge hata mmoja wa upinzani ni sahihi, hili ni lazima tulikate
na tufanye uamuzi huo sasa hasa kuelekea Oktoba mwaka huu,” alisema Zitto.
Akizungumzia Mkoa wa Ruvuma kama mmoja wa mikoa mitano
inayotegemewa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula, alisema pamoja na wakulima
kuhangaika usiku na mchana lakini bado hakuna juhusu za Serikali za kuwakomboa
katika lindi la umaskini ili wafurahie kilimo chao.
Alisema kwa muda sasa bei za mazao zimekuwa zikishuka
lakini bado Serikali imeshindwa kuwalipa wakulima Sh bilioni 13 za mahindi bila
kuwa na utaratibu madhubuti wa kulipa madeni hayo.
“Kwan chi zilizoendelea zimekuwa zikithamini juhudi
zinazofanywa na wakulima ikiwemo kuundiwa mfuko wa mazao, ambao unafanya kazi
ya kuhakikisha dhamani ya mazao inalindwa.
“Ikitoa bei ya mazao inashuka linakua jukumu la mfuko kulipa fidia ya hasara kwa wakulima, ambapo
hili huenda sambamba na kuwepo kwa mfuko huo ambao.
“Nasi ACT- Wazalendo tungependa kuonyesha sera yetu ya
hifadhi ya jamii ambapo kila mkulima awe na bima ya afya. Mpango wetu ni kwamba
kama mchango wa hifadhi ya jamii ni Sh 30,000 basi Serikali itamchangia mkulima
Sh 10,000,” alisema Zitto
Alisema kutokana na changamoto za wakulima wanataka
kuonyesha wana majawabu ambapo mkulima atatibiwa bure akiwa na hifadhi ya jamii
na uhakika wa bei kupitia mfumuko wa bei katika hifadhi ya jamii.
“Utafiti wa Shirikala la Kazi Duniani (ILO), wa mwaka 2013
unaonyesha kuwa nchi ambazo zimesambaza hiafdhi ya jamii kwa wananchi wake wote
zimeondoka kwenye umaskini kwa kasi na ukiaji wa uchumi unaongezeka mara dufu,”
alisema Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo
Mgomo
wa madereva
Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa
kilichotokea jana ni mapambano kati ya wenye nguvu na wanyonge kwani madereva
hawana mikataba ya kazi zao lakini wamiliki wamekuwa wakiwanyonya madereva huku
Serikali iksihindwa kuchukua hatua zozote.
“Hatua za kuimarisha usalama lazima ziendane na usalama wa
ajira za Watanzania katika sekta ya usafirishaji hivyo Serikali ichukue hatua
za haraka kwa kukutana na viongozi wa madereva na kupata suluhisho la kudumu.
“Waziri Samuel Sitta asitishe kwa muda uamuzi wa Serikali
kuhusu mafunzo na Serikali ihakikishe madereva wote wana mikataba ikiwemo
michango kwenye hifadhi ya jamii, Serikali itekeleze uamuzi wa mafunzo.
“Kuna haja ya kuhakikisha kuwa udereva wa mabasi ya abiria
ni taaluma hivyo kuwepo na mfumo wa ‘accredition’ kupitia umoja wa madereva
katika usafirishaji wa umma,” alisema
Zitto alisema ACT-Wazalendo, inasimama upande wa wanyonge
hivyo ipo na madereva wote nchini wanaovuja jasho kuzalisha kwa ajili ya
matajiri wao na pia tunaitaka Serikali imalize tataizo hili mara moja na
wananchi waendelee na shughuli za uzalishaji kama kawaida.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira,
alisema chama chake hakina ugomvi na chama chochote cha siasa nchini na kipo
tayari kushirikiana na chama kinachoamini katika itikadi za kitaifa.
“Ninajua hapa kuna watu wamekuwa wakisema kuwa
ACT-Wazalendo haitaki kushirikiana na vyama vingine hili si kweli kubwa
tunachosema kama kuna chama kinaamini katika misingi ya ujamaa kije
tutashirikiana nao,” alisema Anna.
Kabla yakuwahutubia wananchi mjini hapa viongozi hao wa
ACT-Wazalendo, alisema wakazi wa vitongoji vya mji huo Zitto alifungua matawi
kadhaa ya chama hicho ambapo alielezea mikakati ya chama hicho kuelekea
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Matawi yaliyofunguliwa jana katika eneo la Mshangano,
Bombambili, Msamala kwa Mauki na Lizaboni.
Mbali na kufanya shughuli hizo pia walitembelea makumbusho
ya mashujaa mjini hapa pamoja na kufanya vikao na viongozi wa chama na ngazi ya
mkoa kama njia ya kujiimarisha.
No comments:
Post a Comment