KWA MAWASILIANO ZAIDI: E-mail: yusuf.badi2@gmail.com.

NSSF

TANGAZO

Wednesday, February 27, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM .

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye uwanja wa sherehe baada ya kupata maelezo na kutoa maagizo kwa  uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yake. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia makamanda wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea makao makuu yao
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea
(PICHA NA IKULU)

SHEIKH ALI YOUSEIF AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na  Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Al
Youseif Sheikh Abdullah Mohamed Alyouseif,alipofika Ikulu Mjini
Zanzibar kuonana na Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na   Mwenyekiti wa  Jumuiya
ya Al Youseif Sheikh Abdullah Mohamed Alyouseif,alipofika Ikulu Mjini
Zanzibar kuonana  Rais. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

BINTI ALIYEFANYIWA UNYAMA NA WATU 3 KWA KUFUNGIWA NA KUFICHWA MIEZI 4 NDANI YA CHUMBA KILICHOJENGWA NA MATOFALI KAMA KABURI AMBAMO AKILALA HUMO MCHANA NA USIKU KUCHA.

 Nyumbani kwao Kijijini Kidimu Mkoa wa Pwani.
 Hii ni nyumba (JERA) alikokuwa akiishi  karibu  pembeni ya barabara ya kwenda Bagamoyo.
 Nyumba (JERA) joto na juu vilikuwa vyake.
 Nyumba aliyoishi (JERA) kulikuwa na ulinzi mkali ili asitoloke.
 Shule ya Sekondari anayosoma ni mwanafunzi wa kidato cha 2 pili mwaka huu lakini alichelewa kulipoti kwa sababu ya matatizo hayo.

Akionesha sehemu aliyokuwa akilala mchana kutwa na usiku kucha.
 Bibi akiangalia sehemu mjukuu wake akiishi kwa taabu kwa miezi 4.

 Babu akiwa amekaa katika godoro ambalo lilifunikwa juu kama kitanda chini akilala mjukuu wake.

 Hapo ni kama chaga lakini chini yake ndiyo yalikuwa maisha yake kwa miezi4
Jinsi alivyokuwa akilala baada ya kufunikwa chaga na godoro.

KWA UFUPI
Binti huyu mwenye umri wa  miaka 16 na mwanafunzi wa kidato cha pili 2 alitekwa na Vijana watatu wakati akielekea kanisani mwezi wa 11-2012 na kupatikana baada ya kukimbia tarehe 23/2/2013.  (PICHA NA HABARI NA TANZANIA LIVE BLOG)
 


Tuesday, February 26, 2013

WALIOMTENDEA UNYAMA BINTI HUYU SIYO WATU WA KAWAIDA .


Soma habari hii kwenye gazeti hili,Jioni fuatilia TANZANIA LIVE BLOG utaona mengi zaidi.

MAMA SALMA ATEMBELEA MKOA WA RUKWA.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha akinamama cha Upendo kilichoko katika makao makuu ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai tarehe 26.2.2013. Akinamama hao wapatao kumi hujishughulisha na kazi ya kukamua mafuta ya alizeti.
Mjumbe wa NEC ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha Mafundi seremala kiitwacho Kazimoto kilichoko kaika mji wa Matai wilayani Kalambo.
Mara baada ya kuzindua matawi hayo mawili ya wakererketwa wa CCM, Mama Salma Kikwete anaonekana akiwapungia wananchi waliohudhuria sherehe hiyo huko Matai katika wilaya Kalambo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Matai waliofurika katika eneo la soko jipya mjini hapo ili kushiriki katika sherehe ya kukabidhi pikipiki kumi kwa ajili ya watendaji wa vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa baadhi ya vikundi vilivyoshiriki katika shughuli ya kukabidhi pikipiki kwenye vituo vya afya vya mikoa ya Rukwa na Katavi zilizofanyika huko Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Matai waliohudhuria sherehe ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Matai waliohudhuria sherehe ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi funguo za pikipiki Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Ndugu Paza Mwamlima kwa ajili ya vituo vya afya vya mkoa huo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Pikipiki hizo zimetolewa na kampuni ya Waterrids.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini ndugu Maria Chambanenji, 38, ambaye ni mlemavu wa ngozi kutoka katika kijiji cha Mkoe, Kata ya Mnyangalua wilayani Sumbawanga ambaye alivamiwa na watu wasiojulikana tarehe 10.2.2013 na kumkata mkono wa kushoto. Maria amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Rukwa.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amembeba mtoto Emma, mwenye umri wa miezi minne na nusu, mtoto wa Maria, ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa mkono na watu wasiojulikana wakati walipovamia nyumbani kwake tarehe 10.2.2013. Maria ni mke wa tatu wa Bwana Gabriel Yohana ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani kwa Maria wakati watu hao walipomvamia.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amembeba mtoto Emma, mwenye umri wa miezi minne na nusu, mtoto wa Maria, ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa mkono na watu wasiojulikana wakati walipovamia nyumbani kwake tarehe 10.2.2013. Maria ni mke wa tatu wa Bwana Gabriel Yohana ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani kwa Maria wakati watu hao walipomvamia.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amembeba mtoto Emma, mwenye umri wa miezi minne na nusu, mtoto wa Maria, ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa mkono na watu wasiojulikana wakati walipovamia nyumbani kwake tarehe 10.2.2013. Maria ni mke wa tatu wa Bwana Gabriel Yohana ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani kwa Maria wakati watu hao walipomvamia.
Mbunge wa zamani wa Kwela Ndugu Chrisant Mzindakaya akishiriki kucheza ngoma ya utamaduni ya kabila la Wafipa wakati  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea hospitali ya Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya tiba vyenye thamani ya shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga waliokusanyka katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Theresia.
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wakiangalia baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa  na Mama Salma. (PICHA NA JOHN LUKUWI)


Na Anna Nkinda – Sumbawanga

Watoto wa kike nchini wametakiwa kuepukana na vishawishi vya chips Kuku, lifti, simu za mkononi na zawadi za aina mbalimbali wanazorubuniwa nazo  kwani vitu hivyo havina nia njema ya  kumkomboa msichana kielimu , kijamii na kiuchumi  zaidi ya kumuharibia mpango mzima wa maisha yake.
Onyo hilo limetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanafunzi wa kike zaidi ya 1000 kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Rukwa  katika viwanja vya shule ya Sekondari ya wasichana ya mtakatifu Theresia iliyopo mjini Sumbawanga.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kwamba watoto wengi wa kike wanashindwa kumaliza masomo na kufikia malengo kutokana na changamoto  zinazowakabili ambazo nyingi siyo za kitaaluma japo zinaathali nyingi kitaaluma , kiafya na kimaendeleo.
“Tunafahamu kuwa wanafunzi wengi hupata vishawishi ambavyo huwapelekea kupoteza umakini, muelekeo na kuwa watoro, kupata ujauzito, maambukizi ya Ukimwi na hatimaye kupoteza fursa hii adimu na adhimu ya elimu ya Sekondari na dira ya maisha yao. Ni muhimu kujidhatiti na kujiepusha na mitego, vishawishi na matendo yanayoweza kusababisha matatizo haya.
Msikubali vishawishi kwani peremende ya dakika si sawa na asali ya maisha.Iweje uridhie kuuharibu mpango wa maisha yakokwa kitu cha mara moja? Licha tu ya kuwa atakayehusika na kosa la kukupa mimba anapaswa kushtakiwa kisheria, lakini kwako wewe ni hatari kiafya  kwani kushika mimba ukiwa na umri mdogo unahatarisha maisha yako wakati wa kujifungua. Asilimia ishirini ya vifo vya akina mama wajawazito hutokana na uzazi katika umri mdogo”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwepi pia aliwataka wanafunzi hao kuwatii wazazi wao,kusoma kwa bidii na kujiamini kwamba wanaweza kwani chochote anachoweza kufanya mtoto wa kiume kitaaluma na halikadhalika mtoto wa kike anaweza kukifanya hivyo basi wasome  zaidi masomo ya sayansi na hisabati kama watoto wa kiume.

Akisoma taarifa ya shule ya Sekondari ya wasichana ya Mtakatifu Theresia Sr. Beatrice Cromweli ambaye ni mwalimu alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa na shirika la masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika Jimbo la Sumbawanga mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 85 na hadi sasa kuna wanafunzi 489 na walimu 16.
Alisema kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwa shule hiyo ni kuwaendeleza watoto wa kike kielimu na kimaadili ili kuwakomboa katika unyanyasaji dhidi ya mwanamke na hivyo kuwapa uwezo wa kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao.
Sr. Cromweli alisema,“Shule yetu imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi kila mwaka hii hutokana na ongezeko la vyumba vya madarasa, mabweni ya kulala, vifaa vya kufundishia, walimu na vitendea kazi mbalimbali na ufaulu mzuri wa wanafunzi katika mitihani ya kidato cha nne”.
Alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa vifaa vya maktaba ya kisasa kwani  ujenzi wa jengo  hilo ambalo halijaanza kutumika kikamilifu kutokana na ukosefu wa vitabu, meza, viti na kompyuta umeshakamilika, jengo la bwalo la chakula na ukumbi wa mikutano bado halijakamilika kwani halina meza na viti na uhaba wa vifaa vya maabara ambavyo vinawafanya wanafunzi kutofanya majaribio ya kuridhisha.
Mkoa wa Rukwa umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya  kushuka kwa kiwango cha elimu hasa kwa mtoto wa kike , karibu asilimia 39 ya watoto hao huacha shule kabla ya kumaliza elimu ya  Sekondari kutokana na tatizo la utoro, ujauzito na wazazi kutotilia maanani suala la elimu.

Monday, February 25, 2013

MSHIKEMSHIKE WA MATOKEO KIDATU CHA NNE,VILIO VITUPU,GHARAMA KWA WAZAZI.


WANAFUNZI WALIOSHINDA SHINDANO LA KUANDIKA INSHA.

Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem) Winfrida Leonard kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA – Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki.
Faiza Ussi  kutoka shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki.
Washindi kumi walioshiriki  shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA)  wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.  Wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za kimarekani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki    shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA)  nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa.  Wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla.
Meneja wa shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama  Ali Mindria (kulia) akipokea kombe la ushindi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee kutoka kwa Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) baada ya shule hiyo kuibuka mshindi wa jumla katika   shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA). Wanafunzi wane kutoka shule hiyo waliingia kumi bora kwa kushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa kati ya wanafunzi 32 walioshiriki shindano hilo. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo).

MAMA SALMA AANZA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI RUKWA.

 Mke wa Rais naMwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na mkuu wa Mkoa wa Rukwa mara tu baada ya kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akivishwa skafu na chipukizi mara baada ya kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
 Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea salamu ya heshima kutoka kwa chipukizi wa mkoa wa Rukwa waliofika uwanja wa ndege kumlaki. Mama Salma Kikwete yupo Mkoani  Rukwa kwa ziara ya siku tatu.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Pamoja na mambo mengine Mama Salma atakabidhi vifaa vya tiba katika hospitali ya Mkoa wa Rukwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Pamoja na mambo mengine Mama Salma atakabidhi vifaa vya tiba katika hospitali ya mkoa wa Rukwa. (PICHA NA JOHN LUKUWI)