NSSF
TANGAZO
Thursday, April 18, 2013
MAZIKO YA KAKA YAKE MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMED GHARIB BILAL .
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakilibeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Haji Gharib Bilali, mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal,kabla ya kuswaliwa katika msikiti wa Kilimani Mjini Unguja na kuzikwa Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,akiongoza Swala ya maiti ya Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib
Bilal,katika msikiti wa Kilimani Mjini Zanzibar,ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria katika mazishi hayo Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kushoto waliosimama) Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na wananchi wakiwa katika maziko ya Haji Gharib Bilali,mdogo wake Makamu Dk.Bilal,yaliyofanyika huko Mwera,Wilaya ya Magharibi
Unguja.
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal,akitia udongo katika kaburi la Mdogo wake Marehemu Haji Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali,Mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kushoto waliosimama) Rais wa Jamhuri yaMuungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais wa Jamhuri,Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na wananchi wakiwa katika maziko ya Haji Gharib Bilali,mdogo wake Makamu Dk.Bilal,yaliyofanyika huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
No comments:
Post a Comment