Chemba ya Mtaa wa Libya inamwaga kinyesi baada ya kujaa na kutoshughulikiwa na wahusika kwa muda wa miezi mitatu 3.
Kituo hiki cha Taxi Mitaa hiyo pichani madereva wanakaa kwa ajili ya njaa tu lakini hali ya hapa ni harufu tupu ya kinyesi.
Moja ya duka lililokumbwa na kinyesi kuelea mbele yake Mtaa wa Mkunguni Karibu na Soko la Kisutu,kama unavyoona.
Mtaa wa Libya kuna Bwawa la Kinyesi lililotapakaa na kupelekea barabara kuharibika na kupitika kwa taabu kwa magari yanayopita hapa kwa kipindi cha miezi mitatu.
Mtaa wa Band karibu na Soko la Kisutu hali mbaya kinyesi kimezagaa barabarani na kutoa harufu mbaya sana.
Maji haya yamechanganyika na kinyesi hapa pananuka ukipita unaziba pua kijikinga na harufu.
Hali kama hii ni mbaya kwa Afya za wananchi,wahusika wajibikeni kufanya kazi zenu na siyo kukaa ofisini tu.
No comments:
Post a Comment