Sehemu ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa na mwenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani (kulia),Meneja huduma kwa Wateja,Salome Mallamia na wengine.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani (wapili kushoto) akimtambulisha Mama Salma, Meneja Huduma kwa Wateja,Salome Mallamia na Mkurugenzi wa Ugavi, Missanga Muja (kulia).
Mwenyekitui wa WAMA Mama Salma akitambulishwa viongozi wa (MSD)
Mwenyekitui wa WAMA Mama Salma akitambulishwa viongozi wa (MSD)
Mwenyekiti wa WAMA mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembezwa katika ghara la kuhifadhia Dawa na mwenyeji wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akpewa maelezo na mwenyeji wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu Bohari Kuu ya Dawa (MSD),Cosmas Mwaifwani.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akioneshwa baadhi ya vifaa na Ofisa Mauzo MSD,Yonah Msengi.huku watu wengine wakishuhudia wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akigusa moja ya bosi lenye dawa.
Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya kipimio cha uzito wa mtoto baada ya kuzaliwa cha digito kutoka kwa Ofisa mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD),Yonah Msengi (kulia) Mama alitembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuangalia vifaa vya akina mama vinavyotumika katika kujifungua. Wengine Kaimu Mkurugenzi Mkuu Cosmas Mwaifwani (katikati) na viongozi wengine.
Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya shuka alipotembelea Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia vifaa vya akina mama vinavyotumika wakati wa kujifungua. Kushoto Ofisa Mauzo Yonaha Msengi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Cosmas Mwaifwani (katikati).
Sehemu ya Mabosi yaliyojaa Dawa Bohari Kuu (MSD) Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mabosi yaliyojaa Dawa Bohari Kuu (MSD) Jijini Dar es Salaam.Hakuna shida ya Dawa.
Mwenyekiti wa WAMA akiangalia Dawa ndani ya Ghara.
Mwenyekiti wa WAMA akiangalia Dawa ndani ya Ghara.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akioneshwa vifaa vya kina mama na Ofisa Mauzo Yonaha Msengi.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiangalia vifaa vinavyotumika na akinamama wakati wa kujifungua alipofanya ziara Bohari Kuu ya Dawa Jijini Dar es Salaam.
WAJAWAZITO WAKIJIFUNG
WAJAWAZITO WAKIJIFUNG UA KATIKA MAZINGIRA SALAMA VIFO VYAO VITAPUNGUA - SALMA KIKWETE
Na Anna Nkinda –
Maelezo
Ili
kuhakikisha vifo vya kina mama wajawazito vinapungua ni lazima wajifungue
katika mazingira salama huku kukiwa na upatikanaji wa kutosha wa vifaa tiba.
Hayo yamesemwa jana na
Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akiongea na viongozi
wa Bohari ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alitembelea makao
makuu ya MSD kwa ajili ya kuangalia vifaa tiba ikiwa ni pamoja na vifaa vya
kujifungulia kina mama wajawazito.
Alisema kama mama
atajifungua katika mazingira salama nchi itaweza kuvuka malengo ya milinia ya
kupunguza vifo vya kina mama wajawazito ambavyo kwa sasa vimepungua kutoka 452
kwa kila vizazi hai 100000 hadi kufikia 432 kwa kila vizazi hai 100000 jambo
ambalo litasababisha maisha ya mama kuwa bora.
“Moja ya kazi
zinazofanywa na taasisi ya WAMA ni kuboresha afya ya mama na mtoto hapa nchini,
katika hili tunatoa vifaa tiba vikiwemo vitanda vya kujifungulia kina mama
wajawazito katika Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati ili kuhakikisha kina mama wanajifungua katika
mazingira salama” .
Wakati wa ziara ya Rais
Kikwete mkoani Morogoro niliahidi kutoa
vitanda vya kujifungulia ili kina mama waweze kujifungua salama, nimekuja hapa
na nimejionea vitanda vizuri na vya kisasa vya kujifungulia pamoja na vifaa
vingine ambavyo vinatumika kwa mama mjamzito naahidi nitawapelekea vifaa hivyo”,
alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete pia
aliwataka viongozi hao kuongeza juhudi
katika utendaji wao wa kazi ya
kuokoa maisha ya binadamu na kuhakikisha dawa wanazozipokea zinafika kwa mlaji
kwa wakati kwani kama zitafika kwa wakati vifo vitapungua.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Cosmas Mwaifwani alisema tangu mwaka wa fedha uliopita
wameanza kupeleka dawa na vifaa tiba moja kwa moja katika ngazi ya vituo vya
afya na kuvifikisha kwa mlaji nia ikiwa ni kufikisha huduma hii kwa mlengwa kwa
ubora unaotakiwa na kwa wakati.
“Dhina ya MSD ni kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vyenye
ubora kwa bei naafuu kwa watanzania wote, ndiyo maana tunafika Tanzania nzima
na hata kule ambako kuna ugumu wa kufika zinaangaliwa njia mbadala za kufika
huko”.
Hivi sasa tunaweza
kusimama na kuizungumzia dhina hii bila wasiwasi kwani kwa sasa tafiti
zinaonyesha kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeongezeka kutoka asilimia
45 hadi kufikia asilimia 85”, alisema Mwaifwani.
Alisema pamoja na kwamba
MSD inashughulikia Hospital, Zahanati na Vituo vya afya vya Serikali na taasisi
zilizoidhinishwa na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bado ipo tayari kutoa
huduma kwa makundi mengine ambayo
yanatuma maombi kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa matumizi ya wananchi.
Mwaifwani alisema, “Pale
ambapo kundi la watu ama mtu binafsi anapohitaji vifaa tiba kwa ajili ya
matumizi ya wananchi na vifaa hivyo vikiwepo MSD, hatutakuwa na hiyana ya
kutompatia huduma hiyo kwani tumedhamiria kuokoa maisha ya watanzania”.
Bohari ya Dawa ni moja
ya Idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inajiendsha
chini ya Bodi ya wadhamini yenye majukumu makuu matatu ambayo ni kununua,
kuhifadhi na kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa
Hospitali za Serikali na zile zilizoidhinishwa na wizara.
No comments:
Post a Comment