Na Anna Nkinda – Maelezo
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaotumikishwa
Duniani inafikia milioni 169 kati ya hao wapo wenye umri wa miaka mitano, wanaotoka
katika familia maskini ambao hulazimika kufanya
kazi ili waweze kuishi na hivyo kukoa fursa ya upata elimu na malezi bora.
Kwa upande wa Tanzania asilimia 27.5 ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 17 wanatumikishwa
katika ajira hatarishi zikiwemo za kufanya kazi majumbani, sehemu za starehe,
uvuvi, migodini, mashamba ya tumbaku na machungwa.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandalia
kwa ajili ya kampeni ya kupambana na utumikishwaji wa watoto iliyoandaliwa na International Rescue Committee
(IRC) na kufanyika katika Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam.
Mama Kikwete ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema
utumikishwaji wa mtoto ni hali
inayomkosesha mtoto haki zake za msingi
kama vile elimu, afya, malezi na kutokupata nafasi ya kucheza na watoto
wenzake.
“Utumikishwaji wa mtoto unamadhara makubwa kwa mtoto
mwenyewe, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Kitendo hiki humsababishia mtoto
kuathirika kiakili,kiafya kisaikolojia,kimakuzi na hata katika mazingira mengine
hupelekea kifo chake”.
Pia husababisha umaskini kati ya kizazi hadi kizai, na hivyo
kudidimiza maendeleo ya Taifa. Aidha mtoto anayetumikishwa hukosa ndoto za maisha bora kwa siku za usoni
kwa kuwa alikosa fursa hiyo akiwa mdogo.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alisema mazingira mazuri ya kisera
na kisheria yametayarishwa kwa ajili ya kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji
ukiwemo wa utumikishwaji katika ajira hatarishi kinachotakiwa ni juhudi za
pamoja ili kuhakikisha watoto hawatumikishwi katika jamii.
Akimkaribisha Mama Kikwete ili aweze kuongea na wageni
waliohudhuria hafla hiyo Mkurugenzi wa IRC Tanzania Elijah Okeyo alisema Ili
kukabiliana na tatizo la ajira za watoto mwishoni mwa mwaka 2012 Serikali ya
Marekani kupitia idara ya Kazi iliwapatia dola
milioni 10 kwa ajii ya mradi wa WEKEZA ambao unafanya kazi zake katika wilaya
sita zilizopo katika mikoa ya Tanga na Kigoma.
Kupitia mradi huo watoto 15,000 walitoka katika ajira hizo, walilindwa ili wasiweze
kujihusha na ajira za watoto na kuweza kurudi
shuleni kuendelea na masomo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa IRC wa Kanda ya Afrika ya
Mashariki na Pembe ya Afrika Kurt Tjossem alisema kazi ya kuwasaidia watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi ni ya kila mtu na siyo ya mtu mmoja hivyo bsi wadau
wote wa watoto waendelee kuwekeza katika elimu kwani ndiyo ukombozi wa maisha
ya mtoto.
Alisema inasikitisha kuona mtoto anaacha shule na kwenda
kufanya kazi ili aweze kuongeza kipato cha familia hali hiyo siyo kama
inawaweka mbali na utoto wao bali inawaharibia maisha yao ya baadaye lakini kuna
matumaini kwao ambayo yataanzia kwa jamii yao lakini ili waweze kufanikiwa ni
lazima wadau wote wawaunge mkono.
Licha ya kufanya kazi zake hapa nchini IRC pia inafanya kazi
katika nchi 40 za kuokoa maisha, kuwasadia
watu ili waweze kujenga upya maisha yao, kuwalinda watu ambao maisha yao
yameathiriwa na vita pamoja na majanga ya asili.
No comments:
Post a Comment